WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA KAMPALA WAJERUHIWA AJALI YA BASI LA KATARAMA NA NOAH KAHAMA
Wanafunzi watano kati ya 60 wa Chuo Kikuu cha Kampala nchini Uganda wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Katarama, lenye namba za usajili T 431 EHW, kugonga gari dogo aina ya Noah lenye namba T 533 DJP katika Barabara ya Kahama–Masumbwe, mkoani Shinyanga.



