TANZANIA NI SALAMA,TUKO TAYARI KWA AFCON 2027- KATAMBI


TANZANIA NI SALAMA, TUKO TAYARI KWA AFCON 2027- KATAMBI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobass Katambi amemshukuru sana Dr. Samia Suluhu Hassan Rais wa JM Tanzania kwa uwekezaji mkubwa anaoufanya kwa vyombo vya usalama kwa kutoa mafunzo ya weledi, ununuzi vitendea kazi, na mbinu mpya za ulinzi za kidigitali.
Katambi amesema Tanzania iko salama na imejipanga vizuri sana kiusalama kwa mbinu na mikakati 30 special na salama kutoka ughaibuni, ulimwengu wa kwanza (15 ya wazi na 15 ya siri) kuilinda Nchi. Wizara yake inaendelea kujidhatiti kimikakati, kimedani na kitekinolojia kuhakikisha mashindano ya AFCON PAMOJA BID 2027 yanafanyika kwa usalama mkubwa, amani na ufanisi

Amewahakikishia waandishi wa hanari kuwa vyombo vya ulinzi chini ya Wizara yake vinazingatia na vitaendelea kuzingatia mambo yafuatayo:
1.Kuimarisha ulinzi wa viwanja na maeneo muhimu

Kuweka askari wa kutosha katika viwanja vya michezo, maeneo ya mazoezi, hoteli za timu, viwanja vya ndege na sehemu za mikusanyiko ya mashabiki.

2. Kudhibiti njia za kuingia na kutoka kwa kutumia ukaguzi maalumu wa usalama.

3. Usimamizi mzuri wa umati wa watu
Kutekeleza mipango ya kudhibiti mikusanyiko ili kuzuia msongamano, vurugu na kukanyagana.

4.Kutenga njia za dharura na maeneo salama kwa watazamaji.

5.Uratibu kati ya taasisi mbalimbali,Kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji, Sekta ya Afya, Mamlaka za Serikali za Mitaa na waandaaji wa mashindano pamoja na kamati mbalimbali husika.
6. Mifumo ya udhibiti uhalifu na Kubadilishana taarifa za kiusalama kwa wakati na kufanya mazoezi ya pamoja ya utayari.

7. Kutumia mifumo maalumu ya Ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za kiintelijensia ili kubaini mapema wahalifu, mienendo shuku na vitisho vinavyoweza kujitokeza, ikiwemo uhalifu, wizi, ugaidi, vurugu za mashabiki na uhalifu wa mtandaoni.

8. Kutumia mbinu mpya za kuchukua hatua za kuzuia kabla ya matukio kutokea.

9.Matumizi ya teknolojia kutumia kamera za ulinzi (CCTV), mifumo ya utambuzi wa wahusika, vifaa vya mawasiliano na mifumo ya ufuatiliaji ili kuongeza ufanisi wa operesheni za usalama.

10.Usalama wa wageni na timupamoja na kutoa ulinzi kwa wachezaji, waamuzi, viongozi wa CAF, wageni wa heshima na mashabiki kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na kuhakikisha usafiri wao unakuwa salama wakati wote.

11. Udhibiti wa uhalifu na uvunjifu wa sheria.

Kuchukua hatua dhidi ya wizi, ulanguzi wa tiketi, biashara haramu, matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine vinavyoweza kuvuruga mashindano.

12. Mipango ya dharura na uokoaji
Kuandaa mpango wa kukabiliana na moto, majanga ya asili, dharura za kiafya na matukio mengine yasiyotegemewa.

13. Tutakuwa na vikosi vya uokoaji na huduma za kwanza katika kila eneo la mashindano.

14. Elimu na ushirikishwaji wa wananchi.

Tutaelimisha mashabiki kuhusu sheria za viwanjani, umuhimu wa kudumisha amani na kutoa taarifa za matukio ya kiusalama pamoja na kuendelea kuhamasisha ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya dola.
15. Pamoja na yote hayo tutazingatia viwango vya kimataifa na kuiga mikakati mizuri niliyojifunza Nchi ya Marekani katika maswala ya ulinzi na walivyofanikiwa kiusalama katika World Cup 2026 na kuutekeleza miongozo ya CAF na viwango vya kimataifa vya usalama wa matukio makubwa ya michezo, ikijumuisha tathmini endelevu ya vihatarishi, uratibu wa taasisi mbalimbali na mipango ya dharura.

Kwa ujumla, mafanikio ya usalama wa AFCON tutayafikia kwa ushirikiano mkubwa tulionao vyombo vya dola chini ya usimamizi mahili wa Mhe. Rais Dr. Samia S Hassan na Amiri Jeshi Mkuu, waandaaji wa mashindano, taasisi nyingine za serikali, sekta binafsi na wananchi, ili kuhakikisha mashindano yanafanyika katika mazingira ya amani, utulivu na usalama kwa washiriki na mashabikij wote.

Niwaombe Watanzania na Jumuiya za Kikanda na Kimataifa kuwapuuza mtu,watu,au kikundi kinachichafua Tanzania katika mitandao ya jamii kwa maneno au maandishi kwa maslahi yao binafsi au vikundi ili kuihujumu uchumi, na maendeleo ya jamii na Taifa letu. Mungu ibariki Tanzania.
Previous Post Next Post

نموذج الاتصال