MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WAWASILISHA TAARIFA ZA KATA ZAO

MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA WAWASILISHA TAARIFA ZA KATA ZAO

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa kazi katika kata zao kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, huku wakibainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi katika maeneo yao.

Taarifa hizo zimewasilishwa leo Agosti 12, 2026, wakati wa kikao cha baraza hilo kilichoketi kujadili maendeleo ya wilaya hiyo.
Miongoni mwa maeneo makuu yaliyogusiwa kwenye taarifa hizo ni pamoja na sekta za elimu, afya, maji, pamoja na nishati ya umeme, ambapo madiwani hao wameiomba halmashauri kuweka msukumo wa pekee katika kuzitatua.

Akiongoza kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa, amewaelekeza wataalamu wa halmashauri hiyo, kuzipokea changamoto zote zilizowasilishwa na kuzifanyia kazi kwa haraka ili kuleta tija na maendeleo kwa wananchi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa akizungumza.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa akizungumza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga akizungumza.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akiwa kwenye kikao.
Baraza la Madiwani wilayani Shinyanga likiendelea.
Previous Post Next Post

نموذج الاتصال