Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mwenge wa uhuru umemulika miradi Saba ya Maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambayo yote umepitishwa kutokana na usimamizi mzuri wa miradi, pamoja na kuzingatia ubora unaotakiwa na kugusa maslahi ya wananchi.
Mwenge huo umekimbizwa leo Agosti 20, 2026 kwa kuweka mawe ya msingi, kuzindua, na kufungua katika miradi hiyo.
Akizungumza wakati wa kupokea Mwenge huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, amesema miradi hiyo saba ina thamani ya sh.bilioni 5.4.
Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Wazo Mwang'onda, akizungumza wakati wa kufungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi hiyo, amesema ameridhishwa nayo kwa utekelezaji wake.
Aidha, amewataka pia wananchi kuendelea kuchangia shughuli za maendeleo pamoja na kuanzisha miradi yao wenyewe ikiwamo ujenzi wa Zahanati na kisha serikali itamalizia na kuanza kutoa huduma.
Katika hatua nyingine, amewasihi wananchi kuendelea kudumisha amani ya nchi.
Aidha, miradi iliyopitiwa na Mwenge huo wa uhuru ni ujenzi wa Zahanati ya Shishinulu, Benki ya CRDB Tawi la Tinde, mradi wa Nishati safi shule ya wasichana Tinde, daraja la Usule, mradi wa maji Imesela- Bukene, kikundi cha vijana Didia, ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa sekondari ya Luhumbo, ofisi na kuzindua Klabu ya wapinga Rushwa.
Tags
HABARI