MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI UKIENDELEA DODOMA
Na Marco Maduhu, DODOMA
MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji umeanza leo Februari 12, 2026 jijini Dodoma, ukiwakutanisha wadau wa sekta ya habari na mawasiliano kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuhitimishwa kesho Februari 13, 2026, ukiwa na lengo la kujadili na kutathmini maendeleo ya sekta ya utangazaji pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji wa huduma hususan vijijini.
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Matumizi ya Teknolojia katika kupanua na kuboresha huduma za utangazaji vijijini,” ikilenga kuhimiza ubunifu na matumizi ya teknolojia za kisasa katika kufikisha taarifa kwa wananchi walioko maeneo ya pembezoni.
Katika mkutano huo, mada mbalimbali zinawasilishwa na kujadiliwa, zikilenga kuboresha mazingira ya kazi kwa vyombo vya habari, kuongeza ufanisi wa utangazaji na kuimarisha mchango wa sekta hiyo katika maendeleo ya jamii.
TAZAMA PICHA👇👇
Meneja kitengo cha Utangazaji Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.