UJENZI WA BARABARA DIDIA–SOLWA WARIDHISHA VIONGOZI WA CCM ILOLA

UJENZI WA BARABARA DIDIA–SOLWA WARIDHISHA VIONGOZI ILOLA

Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA

VIONGOZI wa Kamati ya Siasa ya Kata ya Ilola wilayani Shinyanga, wakishirikiana na viongozi wa jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametembelea na kukagua ujenzi wa barabara ya Didia–Solwa katika kipande cha Ilola chenye urefu wa kilomita mbili.

Ziara hiyo iliongozwa na Diwani wa Kata ya Ilol, Mheshimiwa Kisena Fred, ambapo viongozi hao walieleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea, wakibainisha kuwa mradi huo unapaswa kukamilika ifikapo Aprili 10, 2026.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kisena alimtaka mkandarasi anayetekeleza mradi huo kuhakikisha anakamilisha kazi kwa wakati uliopangwa, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuchelewa kutokana na mazingira yaliyopo kuruhusu kazi kuendelea bila vikwazo.

Aidha, diwani huyo aliishukuru Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kumleta mkandarasi kwa wakati, hatua aliyosema itasaidia kuboresha mawasiliano ya barabara kati ya Didia na Solwa kupitia Kata ya Ilola.
Aliongeza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe kutahakikisha inapitika wakati wote wa mwaka, hivyo kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa maeneo hayo.

Kwa upande wao, viongozi wa chama walipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo, huku wakimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mheshimiwa Julius Mtatiro, kwa usimamizi mzuri wa miradi ndani ya wilaya hiyo.

BOFYA HII LINK 👇👇 UONE AWALI UBOVU WA BARABARA HIYO👇👇


Powered by Blogger.