WAANDISHI WA HABARI WA TIJA WAFANYA UTALII WA NDANI MOROGORO


Waandishi wa habari wa Tija wafanya utalii wa ndani Morogoro

Na Marco Maduhu, MOROGORO

WAANDISHI wa habari wa Tija kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaoshiriki programu ya fellowship ya miezi tisa inayosimamiwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na Shirika la International Media Support (IMS), wamefanya utalii wa ndani katika maporomoko ya maji ya Choma mkoani Morogoro.

TAZAMA VIDEO👇👇
Utalii huo umefanyika leo Mei 28, 2026, ikiwa ni sehemu ya kupumzika “Refresh Maind” baada ya mafunzo ya uandishi wa habari wenye tija, yaliyoanza Mei 25 na yanatarajiwa kuhitimishwa kesho Mei 29, 2026.

Baadhi ya waandishi hao akiwamo Elizabeth Tanzania, wamesema, wamefurahi kufanya utalii huo wa ndani, sambamba na kupata nafasi ya kupumzisha akili zao baada ya mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yamejikita katika uandishi wa habari, unaozingatia sheria, matumizi ya data, na usalama wa kidijitali “Digital & Physical Safety of Journalists”.

lengo la mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo waandishi hao katika uandishi wa habari wenye tija kwa jamii.

Powered by Blogger.