MIGOGORO 331 YATATULIWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA LEGAL AID


MIGOGORO 331 YATATULIWA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA LEGAL AID

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KAMPENI ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid inayoendelea mkoani Shinyanga, imeshawafikia wananchi zaidi ya laki tatu na nusu, huku migogoro 2,370 ikipokelewa na 331 kutatuliwa, mingi ikiwa ya ardhi, madai kati ya watu binafsi na taasisi pamoja na matunzo ya watoto.

Hayo yamebainishwa leo Mei 16, 2026 na Mratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga Raulent Bulilo, wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, alipotembelea mabanda ya huduma kwa wananchi.
Amesema kampeni hiyo ilianza Mei 6 mwaka huu, ikiwa na lengo la kuwafikia wananchi wasioweza kumudu gharama za mawakili, kwa kuwapatia elimu na huduma za kisheria bure ,katika masuala ya ndoa, mirathi, ardhi, madai na jinai zote.

Aidha amesema, kupitia kampeni hiyo, hati miliki za ardhi 92 zimetolewa papo kwa papo katika Manispaa ya Shinyanga, huku Kahama zikitolewa hati 25.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, amesema kupitia kampeni hiyo migogoro mingi imetatuliwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, afanye matangazo barabarani kuwatangazia wananchi wajitokeze kwa wingi kutumia fursa hiyo kupata suluhu ya migogoro yao.

Naye Mmoja wa wananchi Mshandete Mussa, amesema amefursahishwa na huduma hiyo ya msaada wa kisheria, na kwamba amepata vyeti vya kuzaliwa vya watoto wake sita kwa muda mchache.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Mratibu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga Raulent Bulilo akizungumza.
Powered by Blogger.