TAKUKURU YAGUSWA NA WATOTO NJITI SHINYANGA YAKABIDHI VIFAA TIBA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imekabidhi vifaa tiba katika Hospitali ya Rufani Mkoa wa Shinyanga, kwa ajili ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati (njiti), ili kuokoa afya zao.

TAZAMA VIDEO👇👇
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Juni 3, 2026 hospitalini hapo, ambapo vifaa hivyo vimekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Crispin Chalamila, kwa Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Luzila John.

Chalamila amesema vifaa hivyo vinatokana na michango ya watumishi, ikiwa ni sehemu ya kufanya matendo ya huruma, na kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha huduma za afya.
“tumekabidhi mashine mbili ambazo ni Radiant Warmer na Phototherapy ambavyo vimenunuliwa kwa michango ya watumishi wa TAKUKURU,” amesema Chalamila.

Kwa upande wake Dk. Luzila, amesema vifaa hivyo ni msaada mkubwa katika kuokoa afya za watoto hao njiti, kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa mkoani humo, na hospitali imekuwa ikipokea watoto wengi wenye changamoto hiyo.

Ametaja takwimu za miezi mitatu iliyopita, kuwa watoto saba waliofikishwa hospitalini hapo walikuwa na uzito wa chini ya kilo moja, huku watoto 70 wakizaliwa wakiwa na uzito wa chini ya kilo 1.5 na kati yao 50 tayari wamesharuhusiwa baada ya kupata matibabu.
Aidha, ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kuguswa na kuchangia maendeleo katika sekta ya afya.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Crispin Chalamila akizungumza.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Donasian Kessy akizungumza.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk.John Luzila akizungumza.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Crispin Chalamila, (kulia), akikabidhi vifaa tiba kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Dk. John Luzila.

Powered by Blogger.